Walemavu Katika Ajira

Watu wenye ulemavu katika jamii wanatakiwa kutotengwa kwenye masuala mbalimbali ya kuliletea Taifa maendeleo hususani suala la ajira ili kuwawezesha kuwaondoa katika hali ya utegemezi na hatimaye kujitegemea wenyewe.

Kuhusiana na suala la haki sawa katika jamii,katibu wa chama cha walemavu mkoani pwani ambaye pia ni afisa ustawi wa jamii Bibi REGINA MBAJI amesema walemavu wanapaswa kupewa fursa zilizo sawia kama watu wengine wasio na ulemavu.

Baadhi ya watu katika jamii,taasisi ama mashirika yamekuwa yakiwanyima fursa hiyo hata kwa wale walemavu wenye elimu zao wakiwatolea visingizio vyenye lengo la kutoajiri kutokana na ulemavu wao.

Kwa hali hiyo inakatisha tamaa hasa kwa wale walemavu waliopata nafasi ya kujiendeleza kielimu kupitia tasnia tofauti nchini.Pia walezi na wazazi walio na watoto wenye ulemavu wawatoe watoto hao bila kuwaficha na kuwaweka ndani pekee kwani kwa kufanya hivyo ni kuwanyima haki zinazostaili kwa watoto wote pasipo kubagua na hata misaada inayotolewa kwa watoto walio na ulemavu hususani katika elimu.

Napenda kuwakumbushia wamiliki wa miundo mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na ofisi binafsi,mahoteli,nyumba za wageni,viwanda kujenga mazingira ya kirafiki yatakayoepusha malalamiko ya kuonekana kutengwa kwa walemavu,kwani yapo maeneo yanayowabana walemavu hasa wa miguu kushindwa kupita kwa uraisi kutokana na hali zao.Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s