Michango ya watoto yatima katika jamii

JAMII imetakiwa kutambua umuhimu wa kuwatunza na kuwalea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwapatia haki zao za msingi ikiwemo elimu vyakula na mavazi.
Wito huo umetolewa na mbunge viti maalum mkoa mpya wa Geita Mh.Vick-Kamata alipotembelea vituo vya kulelea watoto yatima vya Moyo wa Huruma chenye watoto 84 na Lelea chenye watoto 25 vilivyopo wilayani Geita sanjari na kutoa msaada wenye thamani ya shilingi milioni 3 wa vyakula,mavazi na vinywaji kwa watoto hao ili kuwawezesha kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya 2011.


Amesema kuwa ili kuondoa wimbi la watoto wanaoishi mitaani jamii haina budi ya kuwa inajukumu kubwa la kuwatunza,kuwalea  na kuwawezesha kupata elimu itayowasaidia kujikwamua katika maisha yao ya baadae.
Mh.Kamata ametoa msaada wa mafuta ya kupikia lita 60,Sabuni za kufulia,vinyaji,mchele kilo 200,mbuzi wawili,madaftari kalamu na sukari ambapo pia alishiriki na watoto hao kula nao chakula cha mchana katika kusherehekea mwaka mpya.
Kadharika mbunge huyo ametoa pia msaada wa nguo,Unga wa lishe kwa wafungwa na mahabusu wakiwemo watoto wane ambao mamazao wamo katika gereza la Geita pamoja na kuzungumza na wafungwa na mahabusu wa gereza hilo ambapo amejionea msongamo wa mahabusu unaotokana na kucheleweshwa kwa upelezi wa kesi zinazowakabili.
Aidha kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Geita Joseph Msukuma amesema wilaya hiyo inakabiliwa na ongezeko la idadi ya watoto wanaoishi mitaani hali inayotokana na kuongezeka kwa msongamano wa watu katika Mji wa Geita.
Mwenyekiti ameyataka mashirika hayo yanayolea watoto yatima kufanya jitihada za makusudi kwa kushirikiana na Serikali wahisani na mashirika mbalimbali kuwaondoa watoto walioko mitaani na kuwaweka pamoja ili kuweza kuwalea na kuwapatia elimu itayowasaidia  hapo baadae.
Katika kuunga mkono juhudi za mashirika hao za kulea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu mwenyekiti huyo ametoa msaada wa magodoro 25.Mkoa mpya wa Geita unakabiliwa na ongezeko la watoto wa mitaani ambapo zaidi ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu 2000 wanaishi mitaani kutokana na kuongezeka idadi ambapo zaidi ya watu 100,000 wanaishi mjini Geita.Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s