Nafasi za wajane katika familia
Posted: August 3, 2011 Filed under: Wanawake | Tags: tanzania, wajane, wanawake Leave a commentFamila nyingi wanabagua wanawake waliofiwa na waume wao(wajane) na kusema hawana nafasi tena katika familia hiyo na kutopewa nafasi hata ya kujitetea na kutompa ushirikiano wowote kuhusiana na familia iyo.
Asha Zuberi ni miomgoni wa wajane wanaonyimwa nafasi katika familia, alisema tangu kifo cha mume wake Rashid Kasimu hakuwahi tena kupewa nafasi yeyote katika familia iyo ya kasimu kwa masuala yoyote yanayohusiana na familia iyo na kuhesabiwa sio mwanafamilia na kutothaminiwa tena kama mke wa marehemu Rashid.
Alisema hakuweza hata kupewa nafasi ya kutetea haki yake katika kikao cha familia kinachohusiana na mirathi na kutoshirikishwa na chochote kinachoendelea kuhusiana na mali za mume wake.
“Tangu niambiwe sina thamani tena katika familia ya marehemu mume wangu na siwezi kurithi wala kutetea mali yoyote niliyovuna na mume wangu,pamoja na watoto wangu tuliambiwa hatuna chochote cha kumiliki baada ya hapo ndipo nilipohamuwa kuondoka na watoto wangu kwenda kuanza maisha mapya kama haya ya kuomba misaada barabarani ili kuweza kupata ridhiki ya kura pamoja na watoto wangu kuweza kwenda shule”.
Alisema mtoto mmoja wapo wa Asha zuberi,”Baada ya kikao cha mwisho kilichofanyika, baba mkubwa alisema hatuwezi kupewa chochote, kilichobakia sisi watupeleke kijijini tukalime na mama arithiwe na baba mkubwa waishi kama mke na mume, ndipo tulipohamua na mama kuondoka na kwenda kuishi maisha mengine tofauti na mwanzo ambayo tuliyokuwa tukiishi na marehemu baba kwasababu kwa sasa tunaishi maisha ya kimasikini ya kuomba misaada kwa watu”.
Maisha ya mjane huyo na watoto wake yalikuwa hatarishi sana kwa sasa, tofauti na zamazni katika enzi za marehemu mume wake kama walivyojielezea.Inasikitisha sana kuona bado mpaka leo hii kuna baadhi ya familia wanaendekeza mila za zamani za kurithi wake za wadogo zao na hata wa kaka zao na kuwabagua wajane na kuwaona hawanadhamani tena katika familia hiyo baada ya kufariki mume wake.
Recent Comments