Shule za kata na serikali

Shule za kata ni miongoni mwa shule ambazo zinatoa elimu kwa wananchi wa tanzania,na zilizo ongezwa na serikali kwa ajili ya kuinua kiwango cha elimu nchini.Lakini serikali bado hawazipi kipaumbele shule hizo,nasema serikali kwasababu ukifuatilia sana katika shule hizo hamna hata mtoto wa mkubwa hata mmoja katika shule hizo wengi ni wananchi wa kawaida.

Pia serikali ilihaidi kuleta walimu katika shule hizo za kata,lakini mpaka leo haadi iyo haijafanyiwa kazi,na ilikuwa ni haadi nzuri sana katika kuleta maendeleo ya elimu nchini,ingawa hawatomaliza tatizo la walimu nchini lakini itakuwa imesaidia sana,  hasa zile shule  nyingi zilizojengwa vijijini.

Shule hizo licha ya kuwa vijijini zinakabiliwa na mazingira magumu ya kazi. Moja ya matatizo hayo ni ukosefu wa nishati ya umeme, uhaba wa maji na nyumba za kuishi.Matatizo hayo yamekuwa chanzo cha walimu kutokwenda kufundisha kataka shule hizo na kukimbia.

Kiukweli ni kwamba yapo matatizo ambayo yanaweza kumalizwa katika kipindi kifupi hasa hilo la ujenzi wa nyumba za walimu. Hilo wananchi wanaweza kulitekeleza na ndani ya miaka mitano, shule nyingi zikawa hazina tena shida ya nyumba za kuishi walimu.

Lakini tatizo la maji na nishati ya umeme kwa vijiji ambako wanapangiwa walimu hawa litachukua miaka mingi. Hivyo kwa mwalimu anayesubiri huduma hizi muhimu ziwepo ndipo aende kufundisha kwenye shule hizo ina maana atasubiri kwa miongo kadhaa kwani umasikini wa nchi yetu hauwezeshi kwa sasa kila shule kupewa huduma ya umeme.

Baadhi ya nyumba za walimu wa shule za kata vijijini/mikoani.

 


One Comment on “Shule za kata na serikali”

  1. aisha salum says:

    daa watanzania tujaribu kufanya chochote


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s