Nafasi za wajane katika familia

Famila nyingi wanabagua wanawake waliofiwa na waume wao(wajane) na kusema hawana nafasi tena katika familia hiyo na kutopewa nafasi hata ya kujitetea na kutompa ushirikiano wowote kuhusiana na familia iyo.

Asha Zuberi ni miomgoni wa wajane wanaonyimwa nafasi katika familia, alisema tangu kifo cha mume wake Rashid Kasimu hakuwahi tena kupewa nafasi yeyote katika familia iyo ya kasimu kwa masuala yoyote yanayohusiana na familia iyo na kuhesabiwa sio mwanafamilia na kutothaminiwa tena kama mke wa marehemu Rashid.

Alisema hakuweza hata kupewa nafasi ya kutetea haki yake katika kikao cha familia kinachohusiana na mirathi na kutoshirikishwa na chochote kinachoendelea kuhusiana na mali za mume wake.

“Tangu niambiwe sina thamani tena katika familia ya marehemu mume wangu na siwezi kurithi wala kutetea mali yoyote niliyovuna na mume wangu,pamoja na watoto wangu tuliambiwa hatuna chochote cha kumiliki baada ya hapo ndipo nilipohamuwa kuondoka na watoto wangu kwenda kuanza maisha mapya kama haya ya kuomba misaada barabarani ili kuweza kupata ridhiki ya kura pamoja na watoto wangu kuweza kwenda shule”.

Alisema mtoto mmoja wapo wa Asha zuberi,”Baada ya kikao cha mwisho kilichofanyika, baba mkubwa alisema hatuwezi kupewa chochote, kilichobakia sisi watupeleke kijijini tukalime na mama arithiwe na baba mkubwa waishi kama mke na mume, ndipo tulipohamua na mama kuondoka na kwenda kuishi maisha mengine tofauti na mwanzo ambayo tuliyokuwa tukiishi na marehemu baba kwasababu kwa sasa tunaishi maisha ya kimasikini ya kuomba misaada kwa watu”.

Maisha ya mjane huyo na watoto wake yalikuwa hatarishi sana kwa sasa, tofauti na zamazni katika enzi za marehemu mume wake kama walivyojielezea.Inasikitisha sana kuona bado mpaka leo hii kuna baadhi ya familia wanaendekeza mila za zamani za kurithi wake za wadogo zao na hata wa kaka zao na kuwabagua wajane na kuwaona hawanadhamani tena katika familia hiyo baada ya kufariki mume wake.

 

Advertisements

Wajane kupokonywa haki

Wastani wa matatizo 30 yanayohusiana na migogoro ya mirathi na kupokonywa arthi,baada ya wanawake kufiwa na waume wao,yanaripotiwa kila mwaka katika kituo cha msaada wa sheria(Nola)mkoani Iringa,ilifahamika.

Ilielezwa kwamba hali hiyo inatokana kufuatia kushamiri kwa vitendo vya unyanyasaji/ubaguzi kwa wanawake.

Wakili wa Mahakama kuu,kanda ya Iringa,Dismas Mmbando alisema takwimu hizo zinaonyesha kuwa matukio ya unyanyasaji kwa wanawake,ndani ya mkoa huo yamekuwa yakishamiri kutokana na ufahamu mdogo wa jamii kuhusu sheria ya mirathi na wosia.

Mmbando alisema wanawake wengi bado hawajui wafanye nini pale wanaponyanyaswa na kwamba,wanaoweza kuvifikia vituo vya kisheria na kupatiwa msaada ambao huambatana na kuyafikisha mahakamani kuwa na utata,ni wachache ikilinganishwa na hali halisi.

Alifafanua kuwa migogoro hiyo inachomoza kwa kasi kutokana na wanawake kutothaminiwa.


Watoto wa mitaani na mazingira

Imeelezwa kuwa kuna sababu nyingi zinazochangia kuwepo kwa watoto wa mitaani na wale wanaoishi katika mazingira magumu hapa nchini, huku sababu kuu ikielezwa kwamba ni kuanguka kwa uchumi katika familia nyingi.

Watoto kwenye mazingira magumu.

Bado kuna msaada mkubwa unotakiwa kutolewa na jamii,serikari kutokomeaza suala zima la watoto wa mitaani na hawapati misaada kwa jamii na kujishughulisha wenyewe na biashara ndogondogo.


Chanzo cha watoto wa mitaani

WAKATI  nchi za Afrika zilipofanya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, Juni 16 ikiwa ni njia mojawapo ya kuwakumbuka na kuwaenzi watoto wa Afrika Kusini ambao walifanyanyaswa na kubaguliwa na hata kuuawa wakati wa ubaguzi wa rangi, Tanzania inaelezwa kuwa haina takwimu sahihi za watoto wa mitaani.

Kukosekana kwa takwimu hizo kumeelezwa kuwa kunatokana na sababu mbalimbali ikiwamo kuongezeka siku hadi siku kila sehemu kwa watoto hao, hali ambayo inawafanya watendaji wa Serikali wakose takwimu hizo.Pia, inaelezwa kwamba watoto wengine wanaishi katika mazingira magumu  na hatarishi kwa afya zao, lakini bila kutambuliwa.

Wakiwa mitaani huko, watoto hao wamekuwa wakikumbana na mambo mbalimbali yakiwamo kubakwa, kunyanyaswa, kudhalilishwa kijinsia, vitendo wanavyofanyiwa na watu mbalimbali wakiwamo watoto wenzao na hata watu wazima.

Ugomvi wa wazazi kwenye familia,kutowajibika ipasavyo na umaskini ni  sababu mojawapo ya zinazofanya watoto hao kutoroka na kuingia mitaani na kuishi katika mazingira magumu, hali ambayo inaonyesha wazi kuwa, jamii imeshindwa kuwajibika ipasavyo.Watoto hao ambao wanategemewa kuwa viongozi wa baadaye, lakini wanaonekana kuwa na maisha magumu yanayosababisha kukosa elimu, malezi bora jambo ambalo linawafanya waishi katika mazingira hatarishi.

Ili kutatua tatizo hilo, Serikali, jamii na wadau mbalimbali zikiwamo taasisi za kiraia zina wajibu wa kushirikiana  kwa pamoja na ili kuhakikisha kuwa, wanatoa elimu kuhusu suala hilo.Mbali na wadau hao, walimu pia wana nafasi kubwa ya kutoa elimu kwa wazazi na wanafunzi kupiga vita suala la kutupwa watoto,unyanyasaji, ubebaji wa mimba bila ya kujiandaa jambo ambalo linaweza kupunguza kama si kumaliza  tatizo hilo.