Mazingira ya vyoo vya shule mtihani kwa walemavu

Unapozungumzia mazingira mazuri kwa wanafunzi wenye ulemavu hatumaanishi vifaa na mahitaji mengine ya kitaaluma pekee  bali hata miundombinu kama vyumba vya madarasa, vyoo, maktaba, maabara, mabweni na mazingira ya eneo zima la shule

Kufanya hivi ni kuwapa fursa ya wao kujiona kuwa ni sehemu ya jamii hali itakayowapa ari ya kujifunza sambamba na wenzao wasiokuwa na ulemavu.

Hata hivyo, uchunguzi wangu mdogo umebaini kuwa pamoja na nia ya serikali kutaka watoto walemavu wapelekwe shule bado mazingira ya kujifunza katika shule nyingi hayawavutii watoto hawa hali inayosababisha baadhi yao kukacha masomo.

Hivi leo serikali kupitia mipango kama MMEM, MMES na ujenzi wa shule za kata imefanikiwa kujenga shule nyingi kwa lengo la kutoa fursa zaidi kwa vijana wa Tanzania wanaopata elimu katika madaraja mbalimbali.Lakini ujenzi wa shule hizi umekuwa kikwazo kwa baadhi ya watoto kwa kuwa hali zao za kimaumbile zinawapa ugumu kurandana na hali ya mazingira ya shule.

Peter  Nelson anasoma katika shule hiyo alisema kuwa,

“ Shule ya uhuru mchanganyiko amesema mbali na majengo kujengwa magorofa lakini  tatizo kubwa hasa ni vyoo,hivyo maisha yanatuwia vigumu kwa sisi walemavu maana tunashindwa kupanda maghorofa na vyo pia vibovu sana tunakanyaga uchafu wakati wa kenda kujisaidia ”

Amesema shule nyingi zinazojengwa na serikali bado hawaangalii hali yetu kwa mazingira ya vyoo,inasababisha sisi kuugua mara kwa mara.

Zenah Juma pia ni mwanafunzi wa shule hiyo alikuwa na haya ya kusema

“Ni kweli kama alivyosema mwenzangu ujenzi wa vyoo ni tatizo kubwa sana kwetu kwasababu linasababisha tupate maradhi kaka kichocho,kipundupindu hasa kwa sisi walemavu wa miguu tunaotumia mikono kutembelea”.

Kwahiyo serikai inatakiwa kuwa makini na suala zima la ujenzi wa shule unaoendelea kuangalia na walemavu wanapaswa kujengewa vyoo vya kukidhi haja zao,maana hali hiyo ikiendelea walemavu watapata magonjwa mengi na kushindwa kuhudhuria masomo yao.


Baba wa kambo

Mara baada ya tukio hilo baba huyo alikimbizwa zahanati ya karibu na alipatiwa matibabu na kushonwa nyuzi nane katika mchano alioupata dhidi ya mwanae huyo.

Hata hivyo mama wa kijana huyo alidai mume wake ni mkorofi kupita kiasi na hasa akilewa ukorofi unaongezeka na mara kwa Mara hata yeye huwa anapata vipigo kutoka kwa mume wake huyo kutokana na unywaji wa pombe.

MWISHO.


Baba wa kambo

Kutokana na kitendo hicho chakuchelewa kurudi nyumbani kwake na kijana  huyo kuonekana kuchoshwa na hali hiyo alimueleza mama yake  kwa muda huo alichoka na hatoweza kumtayarishia supu hiyo kwa muda huo na kumuahidi angempikia asubuhi.

Jibu hilo hakupendezwa nalo na baba huyo alimsihi amtengenezee supu hiyo na mama huyo kuenndelea kugoma kupika kwa kuwa alichoshwa na  kusumbuliwa usiku na baba yake huyo.

Kijana huyo kwa kuwa alichoshwa na vitendo vya uonevu dhidi  yake alishindwa uvumilivu na kuchukua uamuzi wa ghafla kuchukua chupa na kumtwanga nayo usoni na kumjeruhi baba huyo na kuchanika sehemu za usoni.

ITAENDELEA


Baba wa kambo

Inasemekana baba wa kambo pia ni miongoni mwa wabaguzi wa watoto wao wa kambo na kuwanyanyasa hata wake zao majumbani.

JOSHUA Maiko [16] mkazi wa Kigogo Mburahati, amemjeruhi baba yake wa kambo sehemu za usoni na kupelekea ashonwe nyuzi nane kwa kile alichodai ni kutokana na kuchoshwa na matendo anayomfanyia.

Kijana huyo machachari aliyechoshwa kuona kila uchwao yeye na mama yake mzazi wakiteseka na tabia za baba huyo alichukua uamuzi huo ili kuweza kukomesha tabia ya baba yake.

Kijana huyo alichukua uamuzi huo juzi, baada ya mama yake akiwa katika ugomvi mkubwa ambao ulidaiwa haukuwa na kichwa wala miguuu kwa kile kilichodaiwa kuwa baba huyo alimtaka mama huyo ainuke usiku wa saa 7, ampikie supu wakati anatoka kwenye kinywaji.

ITAENDELEA…….


Sio kwa mama wa kambo tu hata kwa baba wa kambo

Inasemekana kuwa ni wakina mama wa kambo tu lakini kumbe hadi wa kina baba wa kambo wapo.

Mtoto wa miaka mitatu aliyejulikana kwa jina la Abdalah Ibrahimu,amenusurika kufa baada ya kumwagiwa mafuta ya moto na baba yake wa kambo aliyetajwa kwa jina la Kasimu Ramadhani kwa madai kuwa si mtoto wake wa kuzaa.

Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita maeneo ya Magomeni jijini Dar es Salaam ambapo imedaiwa kuwa si mara ya kwanza kwa Bw.Kasimu kutoa adhabu kama hiyo.

Akiongea kwa masikitiko makubwa mama wa mtoto huyo aliyetambulika kwa jina la Fatuma Ramadhani,aliseme kuwa mumewe alichukua hatua hiyo baada ya mzozo na kuamriwa aondoke nyumbani bila sababu.”Mimi na mwanangu tunaishi kwa hofu kubwa kutokana na Kasimu kututishia maisha kila leo,kwa ujumla tupo hatarini,”alisema.

Aidha,mama huyo alidai kilichomshangaza ni kuona polisi wa Kituo cha Magomeni kuja kumchukua mtuhumiwa bila kumfikisha kituoni kwani walimuachia huru.Mtoto Abdalah amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili katika wodi ya watoto na anasaidiwa na majirani.

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni,Charless Kenyela alipohojiwa alisema hakupata taarifa ya tukio hilo lakini alimuagiza Mkuu wa Polisi Magomeni(Wilaya ya Kinondoni)katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kufanya mahojiano na mama huyo.Baada ya kukamilisha kazi hiyo,Bw.Kasimu aliyiwa mbaroni kwa kosa la jinai.

MWISHO…


Mazingira ya shule na walemavu-sehemu ya tatu

KATIKA mizunguko yangu ya kawaida napata nafasi ya kutembelea Shule ya Uhuru Mchanganyiko.Shule ipo maeneo ya Mtaa wa Shaurimoyo na Uhuru jijini Dar es salaam.

Shule hii ina mchanganyiko wa wanafunzi,wenye mahitaji maalum na wa kawaida.Catherine Mwambe ni miongoni mwa walimu wanofundisha katika shule hii,akifundisha wanafunzi wenye mahitaji maalumu tangu ameingia katika shule hii.

Pamoja na moyo wake wa kujitolea kufundisha watoto hao,ansema kuna changamoto nyingi ambazo Serikali inapaswa kuzifanyia kazi kwa nguvu zote.

Catherine anasema katika kutekeleza malengo ya Milenia,Serikali ya Tanzania ilipitisha Sera ya Elimu kwa Wote,kwa lengo la kuhakikisha kuwa watoto wote,bila kujali jinsia zao na afya zao wanapata elimu sawa.

Catherine anafafanua kuwa licha kuwepo kwa mpango huo,sera hiyo haitekelezwi ipasavyo.”Kwa mfano,hivi sasa kuna shule nyingi za kata zinazojengwa na selikali kwa ajili ya watoto ? “Je,ni kweli Serikali imechukua hatua madhubuti kuhakikisha kuwa majengo hayo yanajengwa kwa kuangalia kuwa watoto wenye ulemavu wanayaweza kuyamudu hasa kwa wale wenye ulemavu wa miguu?”,anahoji.

Anasema kwa tatizo lingine kubwa ni huaba wa walimu katika shule nyingi za walemavu,ukiangalia kuna vyuo vingi vinavyotoa mafuzo ya uhalimu nchini lakini hawaletwi katika kufundisha katika shule zenye watoto walemavu.”Si hivyo tu pia kuna baadhi ya wazazi bado wanawaficha watoto wenye ulemavu jambo ambalo huchangia kuwanyima fursa mbalimbali ikiwamo kupata elimu,”anasema.

Anashauri kwamba,ili kukabiliana na changamoto hizo,Serikali na asasi zisizo za kiserikali zielekeze nguvu katika kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata elimu ya kutosha kuhusu malezi ya watoto wenye ulemavu.”kwa kufanya hivyo itawarahisishia walimu kuwafikia watoto wengi,pia Serikali iboreshe mazingira ya upatikanaji wa elimu,hususan kwa watoto hao,”amesema.

MWISHO…