Rushwa ya ngono kwa ajira

Bado kuna baadhi ya watu wanaendeleza rushwa ya ngono hasa maofisini.

Mbunge wa Kawe Halima Mdee amewataka Wasichana kujiamini na kutokutegemea kutoa Rushwa ya Ngono ndipo watimize ndoto zao za kimaisha. Mdee aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na Wanafunzi wa Chuo cha Mwenge wakati akizindua Tawi la Chadema la Chuoni hapo.

Alisema na kuendelea kuwasisitiza hasa wale wahitimu ambao wakimaliza na kuanza kutafuta ajira na kuambiwa kutoa Rushwa ya ngono ndio apate ajira,’Mjifunze kuwa wasomi tumia elimu yako kutimiza ndoto zako,jiamini mtoto wa kike”


Elimu Tanzania inasaidiaje wahitimu?

Miongoni mwa waajiriwa wengi nchini ukifuatilia historia yake ya elimu atakwambia amesomea malisia,uing.Na ndio waliojaa maofisini lakini kwa wale wahitimu waliomaliza hapahapa nchini bado wapo mpaka leo wanatafuta ajira,ukiuliza kwanini atakwambia anavigezo sasa elimu yetu itatusaidia nini?

 


Msaada kwa wazee wasio jiweza

Hapa mjini pia kuna wazee wasiojiweza wanahitaji msaada lakini wanajamii wengi pamoja na serikali hawaangalii suala hili,wengi wamezoea/wanaangalia sana watoto,ni haki sawa kuwaangalia lakini inatakiwa kugusa sehemu zote na sio kubagua.

Baadhi ya wazee wasiojiweza jijini Dar es salaam wakitafuta msaada.


Ajira kwa wahitimu

Wahitimu wananafasi kubwa sana nchini na wanahitaji  haki yaohasa ya kazi endapo wanapo hitimu masomo yao.Lakini inakuwa shida sana kwaoo kwao kuhusu suala zima la kazi.

kwaiyo serikari kama serikali inatakiwa kukaa na kuandaa mipango ya kuwawezesha wahitimu kuweza kupata kazi bila usumbufu kwa ajili ya kukidhi maitaji yao.Pia itakuwa ni faraja kwao kwa kuonekana kuwwa hawatengwi/hawabaguliwi.


Haki ya elimu kwa watoto

Watoto wanahitaji elimu na muda wa kutosha wa kukaa na wazazi wao sio kuwatumikisha

 

Inaonyesha wazai wengi uwanyima watoto haki ya elimu hasa wale watoto ambao waliopotezewa na wazazi,ndugu zao wa karibu,hatima yake ni kuwatumikisha na kupoteza mda mwingi kwa kufanya biashara na sio kwa ajiri ya masomo.


Ajira kwa jamii

Ni jinsi gani inavyoonyesha suala zima la ajira kwa jamii ni bado gumu na tatizo kubwa hapa nchini hasa kwa vijana na watoto(jamii kwa ujumla).

Mmoja wa wajasili amali Bwana Peter Michaeli kwenye hiyo picha “amesema ni bora afanye hiyo kazi ya kukusanya michanga kuliko kukaa hivi hivi kwasababu utafutaji wa ajira nchini ni mgumu sana”

“Ni bora nipokee shilingi elfu mbili kwa siku kuliko kuendelea kutafuta ajira na kuajiriwa kwasababu nimetafuta ajira takribani miaka mitano mpaka sasa sijapata,”alisema Bakari Juma.


Ajira kwa wanawake

Ili kuwahakikishia wanawake haki ya kupewa ajira,idara husika za kitanzania zinatekeleza kwa bidii,”sheria ya kazi”, kupiga marufuku ubaguzi wa kijinsia wakati wa kuajiri watumishi.

Kuwakikishia wanawake wawe na haki ya kimiliki mali na ufundi sawa na wanaume, kuhakikisha kuwa wanaume na wanawake wanafanya kazi ya aina moja na kupata mshahara sawa kupunguza pengo la mapato kati ya wanaume na wanawake na kupanua maeneo ya kuajiri wanawake.

Kukuza shughuli za utoaji huduma ili kuongeza nafasi za ajira kwa wanawake,kutekeleza vizuri sera ya kulinda kazi ya wafanyakazi wanawake, wanawake wa vijijini wana haki sawa na wanaume katika kusaini mkataba wa kulima mshamba,kuendesha uzalishaji,na kupewa ardhi ya kujenga nyumba.

Pia kuwaelekeza na kuwasaidia wanawake wa vijijini wajifunze ufundi wa kikazi ili waweze kufanya shughuli nyingine mbali na kilimo.