Haki ya elimu kwa watoto

Watoto wanahitaji elimu na muda wa kutosha wa kukaa na wazazi wao sio kuwatumikisha

 

Inaonyesha wazai wengi uwanyima watoto haki ya elimu hasa wale watoto ambao waliopotezewa na wazazi,ndugu zao wa karibu,hatima yake ni kuwatumikisha na kupoteza mda mwingi kwa kufanya biashara na sio kwa ajiri ya masomo.

Advertisements

Uamishaji wa walimu ni kushusha kiwango cha elimu

Elimu ni msingi wa maisha yetu.

Wadau wamebaini kuwa changamoto zinazochangia kushuka kwa elimu ni pamoja na uamishaji/ kubadili badili walimu na kuwatoa kutoka shule moja na kwenda shule nyingine.

Hali hiyo imeeelezwa kuwa inachangia kuwepo kwa matabaka mawili ikiwemo la watakaofaulu na watakaofeli katika mitihani yao ndani ya taifa moja kitu ambacho ni hatari kwa Watanzania.

Ester Mahuza ni mwanafunzi wa shule ya Benjamin Mkapa”ni kweli kitendo cha kubadilishiwa walimu ni kuturudisha nyuma kielimu kwasabu alikuwa ananifundisha mwalimu Fatuma wa somo la english namuelewa kutokana na ufundishaji wake, sasa leo aje mwalimu Eliza kutoka shule ya mkoani Tabora atakuja na ufundishaji wake, ni kitendo ambacho kitachukua mda mrefu mimi kumuelewa,”amesema

Asha Bakari ni mwanafunzi”Sio wote tunaouwezo sawa wa kuelewa darasani,mfano,nmemzoea mwalimu Ezekieli wa history alafu uniletee mwalimu juma kutoka shule nyingine sitomuelewa, kitendo ambacho kitanisababisha kuanza kuchukia somo na kuniletea matokeo mabaya kabisa,”amesema.

Kufuatia hali hiyo Serikali imeshauriwa kubeba mzigo wa kugharimia uendeshaji wa elimu hapa nchini ili kukabiliana na changamoto hizo hasa wakati huu wa utandawazi.


Shule za kata na serikali

Shule za kata ni miongoni mwa shule ambazo zinatoa elimu kwa wananchi wa tanzania,na zilizo ongezwa na serikali kwa ajili ya kuinua kiwango cha elimu nchini.Lakini serikali bado hawazipi kipaumbele shule hizo,nasema serikali kwasababu ukifuatilia sana katika shule hizo hamna hata mtoto wa mkubwa hata mmoja katika shule hizo wengi ni wananchi wa kawaida.

Pia serikali ilihaidi kuleta walimu katika shule hizo za kata,lakini mpaka leo haadi iyo haijafanyiwa kazi,na ilikuwa ni haadi nzuri sana katika kuleta maendeleo ya elimu nchini,ingawa hawatomaliza tatizo la walimu nchini lakini itakuwa imesaidia sana,  hasa zile shule  nyingi zilizojengwa vijijini.

Shule hizo licha ya kuwa vijijini zinakabiliwa na mazingira magumu ya kazi. Moja ya matatizo hayo ni ukosefu wa nishati ya umeme, uhaba wa maji na nyumba za kuishi.Matatizo hayo yamekuwa chanzo cha walimu kutokwenda kufundisha kataka shule hizo na kukimbia.

Kiukweli ni kwamba yapo matatizo ambayo yanaweza kumalizwa katika kipindi kifupi hasa hilo la ujenzi wa nyumba za walimu. Hilo wananchi wanaweza kulitekeleza na ndani ya miaka mitano, shule nyingi zikawa hazina tena shida ya nyumba za kuishi walimu.

Lakini tatizo la maji na nishati ya umeme kwa vijiji ambako wanapangiwa walimu hawa litachukua miaka mingi. Hivyo kwa mwalimu anayesubiri huduma hizi muhimu ziwepo ndipo aende kufundisha kwenye shule hizo ina maana atasubiri kwa miongo kadhaa kwani umasikini wa nchi yetu hauwezeshi kwa sasa kila shule kupewa huduma ya umeme.

Baadhi ya nyumba za walimu wa shule za kata vijijini/mikoani.

 


Kushuka kwa elimu nchini

Elimu ni ufunguo wa Maisha bora kwa kila mtanzania,lakini  kauli hii haipewi kipaumbele katika nchi yetu kwasababu unaubaguzi ambao unaendelea nchini bila ya wananchi kujua,tukiangalia kiwango kikubwa kinachosababisha kwa kushuka kwa elimu nchini ni lungha inayotumiwa kufundishia mashuleni.

Wanafunzi wengi nchini wanasema chanzo kikubwa cha kushuka kwa elimu nchini ni lugha inayotumika kufundishiwa  ni kiingereza,kinapewa sana kipaumbele kuliko lugha yetu ya Taifa,na ni tatizo kubwa sana kwa wanafunzi wa kiafrika kuielewa lugha ngeni na kuitumia marakwamara kuliko lugha ya kiafrika(kiswahili) na kusababisha kufeli kwa mitihani na kurudisha nyuma takwimu za ongezeko la elimu.

Chanzo kikubwa cha kushuka kwa elimu nchini ni ubaguzi wa lugha inayotumika nchini,serikali inatakiwa kulizungumzia na kulitolea ufumbuzi na kutoa haki kwa wanafunzi kuhusiana na lugha inayotumika kufundishia mashuleni.

Chanzo kikubwa cha kushuka kwa elimu nchini ni ubaguzi wa lugha.


ELIMU

wanafunzi kijijini

a Africa zipItasikitisha kuona kuna watoto wanapata elimu kwa style hii ndani ya nchi kama Tanzania,nchi yenye vivutio vingi kwa watu wa mataifa mbalimbali,nchi yenye amani tele,nchi yenye madini kama Tanzanite ambayo upatika Tanzania tu,dhahabu na almasi ndio kwao.Mbuga za wanyama kubwo Tanzania,sasa inakuaje Tanzania ni moja ya nchi masikini?a wanyama kubwa Afrika zipo Tanzania.

Elimu

Wanafunzi wakipata elimu katika mazingira magumu,Wakiwamo nchini Tanzania.

Inaonesha tofauti ya mazingira ya ufundishaji wa mjini na wa kijijini nchini.

Kutokana na hizo picha inaonesha bado kuna ubaguzi wa utoaji wa elimu iliyo bora kati ya mijini na vijijini.Nyenzo za ufundishaji vijijini ni duni kuliko za mijini,serikali imeshindwa kabisa kuboresha miundombinu na mazingira ya kutoa elimu itakayo mjenga mwanafunzi wa kijijini katika elimu ya kujitegemea.Mfano mzuri ni pale ambapo vijijini kuna wanafunzi bado wanasomea chini ya miti na wengine majengo mabovu ambayo hayakidhi elimu iliyo bora.