Mazingira ya vyoo vya shule mtihani kwa walemavu

Unapozungumzia mazingira mazuri kwa wanafunzi wenye ulemavu hatumaanishi vifaa na mahitaji mengine ya kitaaluma pekee  bali hata miundombinu kama vyumba vya madarasa, vyoo, maktaba, maabara, mabweni na mazingira ya eneo zima la shule

Kufanya hivi ni kuwapa fursa ya wao kujiona kuwa ni sehemu ya jamii hali itakayowapa ari ya kujifunza sambamba na wenzao wasiokuwa na ulemavu.

Hata hivyo, uchunguzi wangu mdogo umebaini kuwa pamoja na nia ya serikali kutaka watoto walemavu wapelekwe shule bado mazingira ya kujifunza katika shule nyingi hayawavutii watoto hawa hali inayosababisha baadhi yao kukacha masomo.

Hivi leo serikali kupitia mipango kama MMEM, MMES na ujenzi wa shule za kata imefanikiwa kujenga shule nyingi kwa lengo la kutoa fursa zaidi kwa vijana wa Tanzania wanaopata elimu katika madaraja mbalimbali.Lakini ujenzi wa shule hizi umekuwa kikwazo kwa baadhi ya watoto kwa kuwa hali zao za kimaumbile zinawapa ugumu kurandana na hali ya mazingira ya shule.

Peter  Nelson anasoma katika shule hiyo alisema kuwa,

“ Shule ya uhuru mchanganyiko amesema mbali na majengo kujengwa magorofa lakini  tatizo kubwa hasa ni vyoo,hivyo maisha yanatuwia vigumu kwa sisi walemavu maana tunashindwa kupanda maghorofa na vyo pia vibovu sana tunakanyaga uchafu wakati wa kenda kujisaidia ”

Amesema shule nyingi zinazojengwa na serikali bado hawaangalii hali yetu kwa mazingira ya vyoo,inasababisha sisi kuugua mara kwa mara.

Zenah Juma pia ni mwanafunzi wa shule hiyo alikuwa na haya ya kusema

“Ni kweli kama alivyosema mwenzangu ujenzi wa vyoo ni tatizo kubwa sana kwetu kwasababu linasababisha tupate maradhi kaka kichocho,kipundupindu hasa kwa sisi walemavu wa miguu tunaotumia mikono kutembelea”.

Kwahiyo serikai inatakiwa kuwa makini na suala zima la ujenzi wa shule unaoendelea kuangalia na walemavu wanapaswa kujengewa vyoo vya kukidhi haja zao,maana hali hiyo ikiendelea walemavu watapata magonjwa mengi na kushindwa kuhudhuria masomo yao.


Mazingira ya shule na walemavu-sehemu ya tatu

KATIKA mizunguko yangu ya kawaida napata nafasi ya kutembelea Shule ya Uhuru Mchanganyiko.Shule ipo maeneo ya Mtaa wa Shaurimoyo na Uhuru jijini Dar es salaam.

Shule hii ina mchanganyiko wa wanafunzi,wenye mahitaji maalum na wa kawaida.Catherine Mwambe ni miongoni mwa walimu wanofundisha katika shule hii,akifundisha wanafunzi wenye mahitaji maalumu tangu ameingia katika shule hii.

Pamoja na moyo wake wa kujitolea kufundisha watoto hao,ansema kuna changamoto nyingi ambazo Serikali inapaswa kuzifanyia kazi kwa nguvu zote.

Catherine anasema katika kutekeleza malengo ya Milenia,Serikali ya Tanzania ilipitisha Sera ya Elimu kwa Wote,kwa lengo la kuhakikisha kuwa watoto wote,bila kujali jinsia zao na afya zao wanapata elimu sawa.

Catherine anafafanua kuwa licha kuwepo kwa mpango huo,sera hiyo haitekelezwi ipasavyo.”Kwa mfano,hivi sasa kuna shule nyingi za kata zinazojengwa na selikali kwa ajili ya watoto ? “Je,ni kweli Serikali imechukua hatua madhubuti kuhakikisha kuwa majengo hayo yanajengwa kwa kuangalia kuwa watoto wenye ulemavu wanayaweza kuyamudu hasa kwa wale wenye ulemavu wa miguu?”,anahoji.

Anasema kwa tatizo lingine kubwa ni huaba wa walimu katika shule nyingi za walemavu,ukiangalia kuna vyuo vingi vinavyotoa mafuzo ya uhalimu nchini lakini hawaletwi katika kufundisha katika shule zenye watoto walemavu.”Si hivyo tu pia kuna baadhi ya wazazi bado wanawaficha watoto wenye ulemavu jambo ambalo huchangia kuwanyima fursa mbalimbali ikiwamo kupata elimu,”anasema.

Anashauri kwamba,ili kukabiliana na changamoto hizo,Serikali na asasi zisizo za kiserikali zielekeze nguvu katika kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata elimu ya kutosha kuhusu malezi ya watoto wenye ulemavu.”kwa kufanya hivyo itawarahisishia walimu kuwafikia watoto wengi,pia Serikali iboreshe mazingira ya upatikanaji wa elimu,hususan kwa watoto hao,”amesema.

MWISHO…

 

 

 

 

 


Mazingira ya shule na walemavu-sehemu ya pili

Mazingira ni miongoni mwa vitu vya msingi sana katika suala zima la elimu hasa kwa walemavu.Kuna baadhi za shule ambazo zimejengwa na serikali kwa nia ya kutaka watoto walemavu wapelekwe shule,hata hivyo,bado mazingira ya kujifunza katika shule nyingi hayawavutii watoto hawa hali inayosababisha baadhi yao kukacha masomo.

Shule nyingi hasa mijini yamelazimika kujenga majengo ya maghorofa, jambo la kushangaza ujenzi wa majengo haya haukuzingatia mahitaji ya wanafunzi wenye ulemavu hali inyokwanza kuingia na kutoka madarasani kama ilivyo kwa wenzo wasio na ulemavu.

Si majengo ya maghorofa hata zile zilizojengwa chini zikawa na wasaa wa ardhi bado nazo hazikuwakumbuka walemavu.Zipo shule hapa nchini umbali wa kukifuata choo kwa mfano unakaribia mita 100 au 200.Huku ni kuwatesa wanafunzi wenye ulemavu wa miguu.

ENDELEA…..

 

 

 

 

 

 


Mazingira ya shule na walemavu

MWANZONI mwa mwaka 2009,  mke wa Rais,  Salma Kikwete aliitaka jamii kutowatenga wanafunzi wenye ulemavu badala yake wasaidiwe  na kushirikishwa  katika masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo kupewa elimu kama ilivyo kwa makundi mengine ya kijamii.

Siku aliyotoa wito huo hakusita kusema kuwa zaidi ya Sh milioni 881 zinahitajika kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kusomea kwa wanafuzi 8700 wenye ulemavu nchini ili waweze kujifunza katika hali mazingira mazuri.

Tunapozungumzia mazingira mazuri kwa wanafunzi wenye ulemavu hatumaanishi vifaa na mahitaji mengine ya kitaaluma pekee  bali hata miundombinu kama vyumba vya madarasa, vyoo, maktaba, maabara, mabweni na mazingira ya eneo zima la shule

Kufanya hivi ni kuwapa fursa ya wao kujiona kuwa ni sehemu ya jamii hali itakayowapa ari ya kujifunza sambamba na wenzao wasiokuwa na ulemavu.

ENDELEA…………

 


walemavu na elimu

Walemavu pia wanahaki ya kupata elimu ili kuweza kijisaidia katika maisha yake ya baadae.Lakini kuna baadhi ya jamii/familia bado wanawabagua walemavu katika haki yao ya kupata elimu.

Dhamira ya kuamasisha wanafunzi wenye ulemavu katika upatikanaji wa elimu imetokana na ukweli kwamba watu wenye ulemavu hadi sasa wana fursa finyu sana.pamoja na kuwa serikali inatoa miongozo mizuri ya sera na programu kama zile za MMEM na MMES bado programu izi zimeacha nyuma haki za walemavu na elimu kwa kiwango kikubwa.mfano kuna ongezeko kubwa la ujenzi wa madarasa nchi nzima.Lakini madarasa yanayojengwa mengi hayana hata njia za kupita watu wenye ulemavu.Kwa nini?

 

 

 

 


Walemavu kujiwezesha

Walemavu ni binadamu kama wengine na wakijiwezesha wanaweza kuleta mabadiliko nchini na kuliendeleza taifa,lakini kuna baadhi ya wanajamii wanawatenga na kusema ata wakiwezeshwa hawawezi na kuleta dharau kwao na kuwaona hawafahi katika jamii yetu ya leo.

Mlemavu wa miguu mkazi wa Jiji la Arusha, mbaye hakuweza kufahamika jina lake, akiwa katika mitaa ya jiji hilo akitafuta wateja wa biashara yake ya viatu. Watu kama hawa wanahitaji msaada kila kona wanayokuwa wakipita ikiwa ni pamoja na kuwasaidia kuvuka katika barabara, lakini hata hivyo watu kama hawa wakiwezeshwa wanaweza kwani ni watu wangapi wenye viungo vyao kamili na bado wanakaa pembezoni mwa barabara tena katika jiji la Dar es Salaam wakiomba omba tu tena wengine wakiigiza kuwa ni walemavu.


Walemavu Katika Ajira

Watu wenye ulemavu katika jamii wanatakiwa kutotengwa kwenye masuala mbalimbali ya kuliletea Taifa maendeleo hususani suala la ajira ili kuwawezesha kuwaondoa katika hali ya utegemezi na hatimaye kujitegemea wenyewe.

Kuhusiana na suala la haki sawa katika jamii,katibu wa chama cha walemavu mkoani pwani ambaye pia ni afisa ustawi wa jamii Bibi REGINA MBAJI amesema walemavu wanapaswa kupewa fursa zilizo sawia kama watu wengine wasio na ulemavu.

Baadhi ya watu katika jamii,taasisi ama mashirika yamekuwa yakiwanyima fursa hiyo hata kwa wale walemavu wenye elimu zao wakiwatolea visingizio vyenye lengo la kutoajiri kutokana na ulemavu wao.

Kwa hali hiyo inakatisha tamaa hasa kwa wale walemavu waliopata nafasi ya kujiendeleza kielimu kupitia tasnia tofauti nchini.Pia walezi na wazazi walio na watoto wenye ulemavu wawatoe watoto hao bila kuwaficha na kuwaweka ndani pekee kwani kwa kufanya hivyo ni kuwanyima haki zinazostaili kwa watoto wote pasipo kubagua na hata misaada inayotolewa kwa watoto walio na ulemavu hususani katika elimu.

Napenda kuwakumbushia wamiliki wa miundo mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na ofisi binafsi,mahoteli,nyumba za wageni,viwanda kujenga mazingira ya kirafiki yatakayoepusha malalamiko ya kuonekana kutengwa kwa walemavu,kwani yapo maeneo yanayowabana walemavu hasa wa miguu kushindwa kupita kwa uraisi kutokana na hali zao.