Ajira kwa wanawake

Ili kuwahakikishia wanawake haki ya kupewa ajira,idara husika za kitanzania zinatekeleza kwa bidii,”sheria ya kazi”, kupiga marufuku ubaguzi wa kijinsia wakati wa kuajiri watumishi.

Kuwakikishia wanawake wawe na haki ya kimiliki mali na ufundi sawa na wanaume, kuhakikisha kuwa wanaume na wanawake wanafanya kazi ya aina moja na kupata mshahara sawa kupunguza pengo la mapato kati ya wanaume na wanawake na kupanua maeneo ya kuajiri wanawake.

Kukuza shughuli za utoaji huduma ili kuongeza nafasi za ajira kwa wanawake,kutekeleza vizuri sera ya kulinda kazi ya wafanyakazi wanawake, wanawake wa vijijini wana haki sawa na wanaume katika kusaini mkataba wa kulima mshamba,kuendesha uzalishaji,na kupewa ardhi ya kujenga nyumba.

Pia kuwaelekeza na kuwasaidia wanawake wa vijijini wajifunze ufundi wa kikazi ili waweze kufanya shughuli nyingine mbali na kilimo.

 


Nafasi za wajane katika familia

Famila nyingi wanabagua wanawake waliofiwa na waume wao(wajane) na kusema hawana nafasi tena katika familia hiyo na kutopewa nafasi hata ya kujitetea na kutompa ushirikiano wowote kuhusiana na familia iyo.

Asha Zuberi ni miomgoni wa wajane wanaonyimwa nafasi katika familia, alisema tangu kifo cha mume wake Rashid Kasimu hakuwahi tena kupewa nafasi yeyote katika familia iyo ya kasimu kwa masuala yoyote yanayohusiana na familia iyo na kuhesabiwa sio mwanafamilia na kutothaminiwa tena kama mke wa marehemu Rashid.

Alisema hakuweza hata kupewa nafasi ya kutetea haki yake katika kikao cha familia kinachohusiana na mirathi na kutoshirikishwa na chochote kinachoendelea kuhusiana na mali za mume wake.

“Tangu niambiwe sina thamani tena katika familia ya marehemu mume wangu na siwezi kurithi wala kutetea mali yoyote niliyovuna na mume wangu,pamoja na watoto wangu tuliambiwa hatuna chochote cha kumiliki baada ya hapo ndipo nilipohamuwa kuondoka na watoto wangu kwenda kuanza maisha mapya kama haya ya kuomba misaada barabarani ili kuweza kupata ridhiki ya kura pamoja na watoto wangu kuweza kwenda shule”.

Alisema mtoto mmoja wapo wa Asha zuberi,”Baada ya kikao cha mwisho kilichofanyika, baba mkubwa alisema hatuwezi kupewa chochote, kilichobakia sisi watupeleke kijijini tukalime na mama arithiwe na baba mkubwa waishi kama mke na mume, ndipo tulipohamua na mama kuondoka na kwenda kuishi maisha mengine tofauti na mwanzo ambayo tuliyokuwa tukiishi na marehemu baba kwasababu kwa sasa tunaishi maisha ya kimasikini ya kuomba misaada kwa watu”.

Maisha ya mjane huyo na watoto wake yalikuwa hatarishi sana kwa sasa, tofauti na zamazni katika enzi za marehemu mume wake kama walivyojielezea.Inasikitisha sana kuona bado mpaka leo hii kuna baadhi ya familia wanaendekeza mila za zamani za kurithi wake za wadogo zao na hata wa kaka zao na kuwabagua wajane na kuwaona hawanadhamani tena katika familia hiyo baada ya kufariki mume wake.

 


Wajane kupokonywa haki

Wastani wa matatizo 30 yanayohusiana na migogoro ya mirathi na kupokonywa arthi,baada ya wanawake kufiwa na waume wao,yanaripotiwa kila mwaka katika kituo cha msaada wa sheria(Nola)mkoani Iringa,ilifahamika.

Ilielezwa kwamba hali hiyo inatokana kufuatia kushamiri kwa vitendo vya unyanyasaji/ubaguzi kwa wanawake.

Wakili wa Mahakama kuu,kanda ya Iringa,Dismas Mmbando alisema takwimu hizo zinaonyesha kuwa matukio ya unyanyasaji kwa wanawake,ndani ya mkoa huo yamekuwa yakishamiri kutokana na ufahamu mdogo wa jamii kuhusu sheria ya mirathi na wosia.

Mmbando alisema wanawake wengi bado hawajui wafanye nini pale wanaponyanyaswa na kwamba,wanaoweza kuvifikia vituo vya kisheria na kupatiwa msaada ambao huambatana na kuyafikisha mahakamani kuwa na utata,ni wachache ikilinganishwa na hali halisi.

Alifafanua kuwa migogoro hiyo inachomoza kwa kasi kutokana na wanawake kutothaminiwa.


wanawake wanaweza kuleta mabadiliko nchini

kuna baadhi ya wanajamii wanabagua na kutenga wanawake na kusema hawawezi wakati kuna miradi mingi imeanzishwa na wanawake na kuweza kuleta maendeleo nchini au mabadiliko nchini,tukiangalia mkoa wa Ndani kuna kikundi cha wanawake cha miradi mbalimbali ambacho kinasaidia kuleta mabadiliko nchini.

Inaonyesha ni jinsi gani wanawake ni nguvu kazi ya Taifa letu.

Wanawake ni nguvu kazi ya Taifa letu na wanaweza kufanya vitu mbalimbali vya kimaendeleo nchini na sivyo kama baadhi ya wanajamii wanavyowabagua na kusema wanawake ni hasara tu.


wanawake

Katika jamii ya sasa hivi wanawake wanabaguliwa sana kwa kusema hawawezi katika suala zima la kujenga taifa au kuleta maendeleo nchini kwa kusema wanawake wapo kwaajili ya kulea familia nyumbani na sio kufanya kazi za kuendeleza taifa.

Utakuta maofisi mengi wamejaa wanaume na sio wanawake, mabosi wengi ni wanaume kwasababu mpaka umkute bosi mwanamke ujue kampuni yakwake,ata katika famila wakina baba wengi hawapendi wake zao wafanye kazi wanapenda wakae nyumbani tu, na sio kufanya shughuli nyingine,ukiangalia upande wa serikali,  bungeni  wamejaa wanaume na ndio wanaopewa kipaumbele sana katika kutoa hoja.

Naweza kusema wanawake wanaweza kujenga taifa kwasababu wanawake wengi wa jamii ya sasa wanapenda maendeleo ukifuatilia utakuta kuna mitaji,miradi mingi imeanzishwa na wanawake lakini jamii hawalioni hilo, bado baadhi ya wanajamii wanaendeleza mila,tamaduni za zamani kuwa wanawake wapo kwa ajili ya kulea familia tu na sio kuleta maendeleo.

wanawake wakijishughulisha na biashara ndogondogo katika kuendeleza Taifa.

Wanajamii tunatakiwa kuelimika pia baadhi ya wanawake ambao hawajaelimika mpaka sasa waamke na wajitume kwasababu wanawake wanaweza kuinua nchi na kuiletea  maendeleo, msikubali kubaguliwa,watu wote sawa wanawake kwa wanaume kwasababu kazi na shughuli wanazo fanya wanaume, na wanawake wanaweza kwa mfano sasa hivi kuna mafundi umeme wanawake,ujenzi wa nyumba,makonda wa mabasi ya mkoani na daladala.

Ata walio serikarini inawezekana rais kuwa mwanamke mfano mzuri kwasasa  spika wa bunge ni mwanamke,  inatia moyo na inaonyesha wanawake wanaweza na wana nafasi yao katika jamii na kulitumikia taifa.

Wanawake wanaweza kuleta maendeleo ya nchi na kuongoza Taifa.

Kwaiyo ubaguzi katika jamii utokomee tukiwa na umoja katika suala la maendeleo tutafika mbali na kuitangaza nchi na kuleta maendeleo na kuelimisha wasio elimika katika jamii.

Umoja na ushirikiano unaleta maendeleo nchini.