Haki ya elimu kwa watoto

Watoto wanahitaji elimu na muda wa kutosha wa kukaa na wazazi wao sio kuwatumikisha

 

Inaonyesha wazai wengi uwanyima watoto haki ya elimu hasa wale watoto ambao waliopotezewa na wazazi,ndugu zao wa karibu,hatima yake ni kuwatumikisha na kupoteza mda mwingi kwa kufanya biashara na sio kwa ajiri ya masomo.


Ajira


Picha hii ilipigwa mwaka jana na Hassan Mndeme wa Mwananchi   huko mkoani Morogoro katika kijiji cha Komtonga kilichopo wilayani Mvomero. Itazame kwa makini picha yenyewe kisha utafakali unachokiona.Ni ajira kwa watoto,watoto wanacheza,umasikini au nini?Tuambie je tunaweza kuwafanya watoto wetu kuwa taifa la kesho?.


Ajira kwa watoto

Miongoni mwa wazazi wengi wanapenda kuwatumikisha watoto kwa ajiri ya ajira zao ndogondogo za kuweza kukithi mahitaji ya nyumbani kwao ya kila siku.
Juma Bakari ni mtoto mwenye umri wa miaka tisa(9)”ni mtoto wa pili katika familia yangu,ninasoma darasa la tatu katika shule ya msingi kinondoni mda mwingi natumia kufanya biashara ya mama yangu ili tuweze kula baada ya kuuza bisahara ya mama yangu naenda kwenye biashara yangu nimeajiriwa na mama wa jirani kuuza mabarafu na maji utakuta mda mwingine siendi shule au ata nikienda shule nawaza ajira yangu”amesema.
“Ajira nyingi za watoto zinawanyima muda wa kusoma na ata pia zinaleta madhara kwa watoto kwasabu watoto wengi wanakuwa na viburi kwa wakubwa zao”amesema Zuberi Rashidi.


Baba wa kambo

Mara baada ya tukio hilo baba huyo alikimbizwa zahanati ya karibu na alipatiwa matibabu na kushonwa nyuzi nane katika mchano alioupata dhidi ya mwanae huyo.

Hata hivyo mama wa kijana huyo alidai mume wake ni mkorofi kupita kiasi na hasa akilewa ukorofi unaongezeka na mara kwa Mara hata yeye huwa anapata vipigo kutoka kwa mume wake huyo kutokana na unywaji wa pombe.

MWISHO.


Baba wa kambo

Kutokana na kitendo hicho chakuchelewa kurudi nyumbani kwake na kijana  huyo kuonekana kuchoshwa na hali hiyo alimueleza mama yake  kwa muda huo alichoka na hatoweza kumtayarishia supu hiyo kwa muda huo na kumuahidi angempikia asubuhi.

Jibu hilo hakupendezwa nalo na baba huyo alimsihi amtengenezee supu hiyo na mama huyo kuenndelea kugoma kupika kwa kuwa alichoshwa na  kusumbuliwa usiku na baba yake huyo.

Kijana huyo kwa kuwa alichoshwa na vitendo vya uonevu dhidi  yake alishindwa uvumilivu na kuchukua uamuzi wa ghafla kuchukua chupa na kumtwanga nayo usoni na kumjeruhi baba huyo na kuchanika sehemu za usoni.

ITAENDELEA


Baba wa kambo

Inasemekana baba wa kambo pia ni miongoni mwa wabaguzi wa watoto wao wa kambo na kuwanyanyasa hata wake zao majumbani.

JOSHUA Maiko [16] mkazi wa Kigogo Mburahati, amemjeruhi baba yake wa kambo sehemu za usoni na kupelekea ashonwe nyuzi nane kwa kile alichodai ni kutokana na kuchoshwa na matendo anayomfanyia.

Kijana huyo machachari aliyechoshwa kuona kila uchwao yeye na mama yake mzazi wakiteseka na tabia za baba huyo alichukua uamuzi huo ili kuweza kukomesha tabia ya baba yake.

Kijana huyo alichukua uamuzi huo juzi, baada ya mama yake akiwa katika ugomvi mkubwa ambao ulidaiwa haukuwa na kichwa wala miguuu kwa kile kilichodaiwa kuwa baba huyo alimtaka mama huyo ainuke usiku wa saa 7, ampikie supu wakati anatoka kwenye kinywaji.

ITAENDELEA…….


Sio kwa mama wa kambo tu hata kwa baba wa kambo

Inasemekana kuwa ni wakina mama wa kambo tu lakini kumbe hadi wa kina baba wa kambo wapo.

Mtoto wa miaka mitatu aliyejulikana kwa jina la Abdalah Ibrahimu,amenusurika kufa baada ya kumwagiwa mafuta ya moto na baba yake wa kambo aliyetajwa kwa jina la Kasimu Ramadhani kwa madai kuwa si mtoto wake wa kuzaa.

Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita maeneo ya Magomeni jijini Dar es Salaam ambapo imedaiwa kuwa si mara ya kwanza kwa Bw.Kasimu kutoa adhabu kama hiyo.

Akiongea kwa masikitiko makubwa mama wa mtoto huyo aliyetambulika kwa jina la Fatuma Ramadhani,aliseme kuwa mumewe alichukua hatua hiyo baada ya mzozo na kuamriwa aondoke nyumbani bila sababu.”Mimi na mwanangu tunaishi kwa hofu kubwa kutokana na Kasimu kututishia maisha kila leo,kwa ujumla tupo hatarini,”alisema.

Aidha,mama huyo alidai kilichomshangaza ni kuona polisi wa Kituo cha Magomeni kuja kumchukua mtuhumiwa bila kumfikisha kituoni kwani walimuachia huru.Mtoto Abdalah amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili katika wodi ya watoto na anasaidiwa na majirani.

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni,Charless Kenyela alipohojiwa alisema hakupata taarifa ya tukio hilo lakini alimuagiza Mkuu wa Polisi Magomeni(Wilaya ya Kinondoni)katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kufanya mahojiano na mama huyo.Baada ya kukamilisha kazi hiyo,Bw.Kasimu aliyiwa mbaroni kwa kosa la jinai.

MWISHO…