Rushwa ya ngono kwa ajira

Bado kuna baadhi ya watu wanaendeleza rushwa ya ngono hasa maofisini.

Mbunge wa Kawe Halima Mdee amewataka Wasichana kujiamini na kutokutegemea kutoa Rushwa ya Ngono ndipo watimize ndoto zao za kimaisha. Mdee aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na Wanafunzi wa Chuo cha Mwenge wakati akizindua Tawi la Chadema la Chuoni hapo.

Alisema na kuendelea kuwasisitiza hasa wale wahitimu ambao wakimaliza na kuanza kutafuta ajira na kuambiwa kutoa Rushwa ya ngono ndio apate ajira,’Mjifunze kuwa wasomi tumia elimu yako kutimiza ndoto zako,jiamini mtoto wa kike”


Ajira kwa wahitimu

Wahitimu wananafasi kubwa sana nchini na wanahitaji  haki yaohasa ya kazi endapo wanapo hitimu masomo yao.Lakini inakuwa shida sana kwaoo kwao kuhusu suala zima la kazi.

kwaiyo serikari kama serikali inatakiwa kukaa na kuandaa mipango ya kuwawezesha wahitimu kuweza kupata kazi bila usumbufu kwa ajili ya kukidhi maitaji yao.Pia itakuwa ni faraja kwao kwa kuonekana kuwwa hawatengwi/hawabaguliwi.


Ajira kwa jamii

Ni jinsi gani inavyoonyesha suala zima la ajira kwa jamii ni bado gumu na tatizo kubwa hapa nchini hasa kwa vijana na watoto(jamii kwa ujumla).

Mmoja wa wajasili amali Bwana Peter Michaeli kwenye hiyo picha “amesema ni bora afanye hiyo kazi ya kukusanya michanga kuliko kukaa hivi hivi kwasababu utafutaji wa ajira nchini ni mgumu sana”

“Ni bora nipokee shilingi elfu mbili kwa siku kuliko kuendelea kutafuta ajira na kuajiriwa kwasababu nimetafuta ajira takribani miaka mitano mpaka sasa sijapata,”alisema Bakari Juma.


Ajira kwa wanawake

Ili kuwahakikishia wanawake haki ya kupewa ajira,idara husika za kitanzania zinatekeleza kwa bidii,”sheria ya kazi”, kupiga marufuku ubaguzi wa kijinsia wakati wa kuajiri watumishi.

Kuwakikishia wanawake wawe na haki ya kimiliki mali na ufundi sawa na wanaume, kuhakikisha kuwa wanaume na wanawake wanafanya kazi ya aina moja na kupata mshahara sawa kupunguza pengo la mapato kati ya wanaume na wanawake na kupanua maeneo ya kuajiri wanawake.

Kukuza shughuli za utoaji huduma ili kuongeza nafasi za ajira kwa wanawake,kutekeleza vizuri sera ya kulinda kazi ya wafanyakazi wanawake, wanawake wa vijijini wana haki sawa na wanaume katika kusaini mkataba wa kulima mshamba,kuendesha uzalishaji,na kupewa ardhi ya kujenga nyumba.

Pia kuwaelekeza na kuwasaidia wanawake wa vijijini wajifunze ufundi wa kikazi ili waweze kufanya shughuli nyingine mbali na kilimo.

 


Ajira


Picha hii ilipigwa mwaka jana na Hassan Mndeme wa Mwananchi   huko mkoani Morogoro katika kijiji cha Komtonga kilichopo wilayani Mvomero. Itazame kwa makini picha yenyewe kisha utafakali unachokiona.Ni ajira kwa watoto,watoto wanacheza,umasikini au nini?Tuambie je tunaweza kuwafanya watoto wetu kuwa taifa la kesho?.


Ajira kwa vijana

Wachunguzi wa mambo wanasema, kwa hakika ukosefu wa fursa za ajira na umaskini ni kati ya changamoto kubwa miongoni mwa vijana, lakini madai ya kutaifisha migodi pamoja na lugha zinazoashiria ubaguzi ni mambo ambayo kamwe hayawezi kuvumiliwa nchini Afrika ya Kusini, nchi ambayo imepitia vipindi vigumu vya historia yake, hadi sasa walau mafanikio yanaanza kuonekana ikilinganishwa na miaka kadhaa iliyopita.

Ule wimbo wa ajira kwa vijana unaendelea kuimbwa kila siku na sasa umekuwa kero masikioni mwa watanzania. Katika kampeni nyingi za kuwania uongozi au katika majukwaa ya kisiasa,ajenda hii imekuwa ndio mtaji kwa viongozi ili wapate kura. Ahadi nyingi zimetolewa na viongozi huku wakijua kuwa ni uongo hakuna la maana wanalolifanya kutatua hili tatizo la ukosefu wa ajira,hususani kwa vijana.

Ajira 1,000,000 zilizo ahidiwa miaka mingi iliyopita bado ni kitendawili.Kuna kipindi raisi alipokuwa anatoa hotuba kwa taifa kwa njia ya televisheni alisema ajira alizokuwa anazungumzia ni pale mtu anapoanzisha baa, atatoa ajira kwa vijana wale watakao kuwa wanazibua vizibo vya chupa. Ni jambo la kusikitisha mkuu wa nchi kusema neno kama hilo kwa umma wa watanzania.


Walemavu Katika Ajira

Watu wenye ulemavu katika jamii wanatakiwa kutotengwa kwenye masuala mbalimbali ya kuliletea Taifa maendeleo hususani suala la ajira ili kuwawezesha kuwaondoa katika hali ya utegemezi na hatimaye kujitegemea wenyewe.

Kuhusiana na suala la haki sawa katika jamii,katibu wa chama cha walemavu mkoani pwani ambaye pia ni afisa ustawi wa jamii Bibi REGINA MBAJI amesema walemavu wanapaswa kupewa fursa zilizo sawia kama watu wengine wasio na ulemavu.

Baadhi ya watu katika jamii,taasisi ama mashirika yamekuwa yakiwanyima fursa hiyo hata kwa wale walemavu wenye elimu zao wakiwatolea visingizio vyenye lengo la kutoajiri kutokana na ulemavu wao.

Kwa hali hiyo inakatisha tamaa hasa kwa wale walemavu waliopata nafasi ya kujiendeleza kielimu kupitia tasnia tofauti nchini.Pia walezi na wazazi walio na watoto wenye ulemavu wawatoe watoto hao bila kuwaficha na kuwaweka ndani pekee kwani kwa kufanya hivyo ni kuwanyima haki zinazostaili kwa watoto wote pasipo kubagua na hata misaada inayotolewa kwa watoto walio na ulemavu hususani katika elimu.

Napenda kuwakumbushia wamiliki wa miundo mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na ofisi binafsi,mahoteli,nyumba za wageni,viwanda kujenga mazingira ya kirafiki yatakayoepusha malalamiko ya kuonekana kutengwa kwa walemavu,kwani yapo maeneo yanayowabana walemavu hasa wa miguu kushindwa kupita kwa uraisi kutokana na hali zao.