Shule za kata na serikali

Shule za kata ni miongoni mwa shule ambazo zinatoa elimu kwa wananchi wa tanzania,na zilizo ongezwa na serikali kwa ajili ya kuinua kiwango cha elimu nchini.Lakini serikali bado hawazipi kipaumbele shule hizo,nasema serikali kwasababu ukifuatilia sana katika shule hizo hamna hata mtoto wa mkubwa hata mmoja katika shule hizo wengi ni wananchi wa kawaida.

Pia serikali ilihaidi kuleta walimu katika shule hizo za kata,lakini mpaka leo haadi iyo haijafanyiwa kazi,na ilikuwa ni haadi nzuri sana katika kuleta maendeleo ya elimu nchini,ingawa hawatomaliza tatizo la walimu nchini lakini itakuwa imesaidia sana,  hasa zile shule  nyingi zilizojengwa vijijini.

Shule hizo licha ya kuwa vijijini zinakabiliwa na mazingira magumu ya kazi. Moja ya matatizo hayo ni ukosefu wa nishati ya umeme, uhaba wa maji na nyumba za kuishi.Matatizo hayo yamekuwa chanzo cha walimu kutokwenda kufundisha kataka shule hizo na kukimbia.

Kiukweli ni kwamba yapo matatizo ambayo yanaweza kumalizwa katika kipindi kifupi hasa hilo la ujenzi wa nyumba za walimu. Hilo wananchi wanaweza kulitekeleza na ndani ya miaka mitano, shule nyingi zikawa hazina tena shida ya nyumba za kuishi walimu.

Lakini tatizo la maji na nishati ya umeme kwa vijiji ambako wanapangiwa walimu hawa litachukua miaka mingi. Hivyo kwa mwalimu anayesubiri huduma hizi muhimu ziwepo ndipo aende kufundisha kwenye shule hizo ina maana atasubiri kwa miongo kadhaa kwani umasikini wa nchi yetu hauwezeshi kwa sasa kila shule kupewa huduma ya umeme.

Baadhi ya nyumba za walimu wa shule za kata vijijini/mikoani.

 

Advertisements

walemavu na elimu

Walemavu pia wanahaki ya kupata elimu ili kuweza kijisaidia katika maisha yake ya baadae.Lakini kuna baadhi ya jamii/familia bado wanawabagua walemavu katika haki yao ya kupata elimu.

Dhamira ya kuamasisha wanafunzi wenye ulemavu katika upatikanaji wa elimu imetokana na ukweli kwamba watu wenye ulemavu hadi sasa wana fursa finyu sana.pamoja na kuwa serikali inatoa miongozo mizuri ya sera na programu kama zile za MMEM na MMES bado programu izi zimeacha nyuma haki za walemavu na elimu kwa kiwango kikubwa.mfano kuna ongezeko kubwa la ujenzi wa madarasa nchi nzima.Lakini madarasa yanayojengwa mengi hayana hata njia za kupita watu wenye ulemavu.Kwa nini?

 

 

 

 


Kushuka kwa elimu nchini

Elimu ni ufunguo wa Maisha bora kwa kila mtanzania,lakini  kauli hii haipewi kipaumbele katika nchi yetu kwasababu unaubaguzi ambao unaendelea nchini bila ya wananchi kujua,tukiangalia kiwango kikubwa kinachosababisha kwa kushuka kwa elimu nchini ni lungha inayotumiwa kufundishia mashuleni.

Wanafunzi wengi nchini wanasema chanzo kikubwa cha kushuka kwa elimu nchini ni lugha inayotumika kufundishiwa  ni kiingereza,kinapewa sana kipaumbele kuliko lugha yetu ya Taifa,na ni tatizo kubwa sana kwa wanafunzi wa kiafrika kuielewa lugha ngeni na kuitumia marakwamara kuliko lugha ya kiafrika(kiswahili) na kusababisha kufeli kwa mitihani na kurudisha nyuma takwimu za ongezeko la elimu.

Chanzo kikubwa cha kushuka kwa elimu nchini ni ubaguzi wa lugha inayotumika nchini,serikali inatakiwa kulizungumzia na kulitolea ufumbuzi na kutoa haki kwa wanafunzi kuhusiana na lugha inayotumika kufundishia mashuleni.

Chanzo kikubwa cha kushuka kwa elimu nchini ni ubaguzi wa lugha.


ELIMU

wanafunzi kijijini

a Africa zipItasikitisha kuona kuna watoto wanapata elimu kwa style hii ndani ya nchi kama Tanzania,nchi yenye vivutio vingi kwa watu wa mataifa mbalimbali,nchi yenye amani tele,nchi yenye madini kama Tanzanite ambayo upatika Tanzania tu,dhahabu na almasi ndio kwao.Mbuga za wanyama kubwo Tanzania,sasa inakuaje Tanzania ni moja ya nchi masikini?a wanyama kubwa Afrika zipo Tanzania.

Elimu

Wanafunzi wakipata elimu katika mazingira magumu,Wakiwamo nchini Tanzania.

Inaonesha tofauti ya mazingira ya ufundishaji wa mjini na wa kijijini nchini.

Kutokana na hizo picha inaonesha bado kuna ubaguzi wa utoaji wa elimu iliyo bora kati ya mijini na vijijini.Nyenzo za ufundishaji vijijini ni duni kuliko za mijini,serikali imeshindwa kabisa kuboresha miundombinu na mazingira ya kutoa elimu itakayo mjenga mwanafunzi wa kijijini katika elimu ya kujitegemea.Mfano mzuri ni pale ambapo vijijini kuna wanafunzi bado wanasomea chini ya miti na wengine majengo mabovu ambayo hayakidhi elimu iliyo bora.