Sio kwa mama wa kambo tu hata kwa baba wa kambo

Inasemekana kuwa ni wakina mama wa kambo tu lakini kumbe hadi wa kina baba wa kambo wapo.

Mtoto wa miaka mitatu aliyejulikana kwa jina la Abdalah Ibrahimu,amenusurika kufa baada ya kumwagiwa mafuta ya moto na baba yake wa kambo aliyetajwa kwa jina la Kasimu Ramadhani kwa madai kuwa si mtoto wake wa kuzaa.

Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita maeneo ya Magomeni jijini Dar es Salaam ambapo imedaiwa kuwa si mara ya kwanza kwa Bw.Kasimu kutoa adhabu kama hiyo.

Akiongea kwa masikitiko makubwa mama wa mtoto huyo aliyetambulika kwa jina la Fatuma Ramadhani,aliseme kuwa mumewe alichukua hatua hiyo baada ya mzozo na kuamriwa aondoke nyumbani bila sababu.”Mimi na mwanangu tunaishi kwa hofu kubwa kutokana na Kasimu kututishia maisha kila leo,kwa ujumla tupo hatarini,”alisema.

Aidha,mama huyo alidai kilichomshangaza ni kuona polisi wa Kituo cha Magomeni kuja kumchukua mtuhumiwa bila kumfikisha kituoni kwani walimuachia huru.Mtoto Abdalah amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili katika wodi ya watoto na anasaidiwa na majirani.

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni,Charless Kenyela alipohojiwa alisema hakupata taarifa ya tukio hilo lakini alimuagiza Mkuu wa Polisi Magomeni(Wilaya ya Kinondoni)katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kufanya mahojiano na mama huyo.Baada ya kukamilisha kazi hiyo,Bw.Kasimu aliyiwa mbaroni kwa kosa la jinai.

MWISHO…

Advertisements