Wafanyakazi wa ndani katika mishahara

Mfanyakazi/Wafanyakazi wa ndani ni binadamu kama watu wengine,lakini kuna baadhi ya familia wanazoishi na wafanyakazi hao hawawatendei haki(huwabagua),hasa upande wa mishahara yao wengine hawalipwi kabisa na wengine ni midogo.

Celina Christofa ni mmoja wa wafanyakazi wa ndani ambaye ulipwa mshahara mdogo amesema”nalipwa shilingi Elfu kumi na tano kwa mwenzi kwasababu nakura na kulala hapo hapo,kutokana na hali hiyo nikaamua kwenda kulala kwa jirani ili niongezewe mshahara lakini nikawa nachereweshewa kulipwa”.

Hayo ndiyo maisha ya msichana huyo anayoishi ili kukidhi mahitaji yake na familia yake,wanafamilia ambazo wanaishi na wasichana hao wanatakiwa kuwapa haki zao kama wafanyakazi wengine wa maofisini.

Bibi Fatuma Mbwana”Mimi ni jirani yake Celina naona jinsi gani anavyotendewa binti huyu nimeshaongea sana na familia anyoishi nayo celina lakini kila leo naona hali ni ileile,kama mzazi nasema tujitaidi kuwajali mabinti zetu wa ndani kama watoto wetu kwasababu hali hii hikiendelea¬† hinasababisha kuongezeka kwa watoto mitahani na mimba katika umri mdogo”alisema.