Watu wa hali ya chini(Masikini)

Watu tofauti hutafsiri maana ya umasikini kwa njia mbalimbali. Viongozi kwa kawaida hufikiria juu ya umasikini kwa kuangalia uwezo wa watu katika kununua mahitaji yao na kuuza bidhaa zao. Lakini tafsiri ya umasikini ni kubwa zaidi. Kuna tafsiri ya kuzingatia matatizo ya kuwa na mgawanyo sawa katika kupata elimu na afya bora, kuwa na heshima na hadhi katika jamii, kujisikia kuwa una uwezo wa kutatua tatizo lolote linalotokea katika maisha yako, na hivyo kuwa na matumaini ya maisha. Kwa hakika fikra nyingi haziko wazi mpaka unapofikiria kwa makini yanayotendeka katika jamii.

Pia wengine hufikilia watu wa hali ya chini ni watu wasio na ajira,walioacha shule,madereva wa teksi na wapanda pikipiki,wahamiaji,waombaji,wafanyakazi wa bandari,makuli,na wafanyakazi wajezi.Lakini watu hawa hawa wa hali ya chini bado kuna baadhi ya wanajamii wanawabagua na kuwadharau na bila kufikila kuwa hao watu wa hali ya chini ni tegemezi la taifa letu.

Kwasababu kutokana na makundi mbalimbali ya watu wa chini kama wafanyakazi wajenzi ni nguvu kazi tosha ya taifa letu ambalo hutumika katika ujenzi wa taifa nchini lakini bado hawahonekani katika jamii kama wanahumuhimu hatima yake kubaguliwa na kutengwa na kuchekwa na kuitwa masikini.

Kwaiyo jamii na taifa kwa ujumla inatakiwa kuwafikilia watu wa hali ya chini na kutafuta humuhimu wao na sio kuwatenga na kuwachukulia kuwa hawana humuhimu wowote katika jamii yetu.