Wafanyakazi wa ndani katika mishahara

Mfanyakazi/Wafanyakazi wa ndani ni binadamu kama watu wengine,lakini kuna baadhi ya familia wanazoishi na wafanyakazi hao hawawatendei haki(huwabagua),hasa upande wa mishahara yao wengine hawalipwi kabisa na wengine ni midogo.

Celina Christofa ni mmoja wa wafanyakazi wa ndani ambaye ulipwa mshahara mdogo amesema”nalipwa shilingi Elfu kumi na tano kwa mwenzi kwasababu nakura na kulala hapo hapo,kutokana na hali hiyo nikaamua kwenda kulala kwa jirani ili niongezewe mshahara lakini nikawa nachereweshewa kulipwa”.

Hayo ndiyo maisha ya msichana huyo anayoishi ili kukidhi mahitaji yake na familia yake,wanafamilia ambazo wanaishi na wasichana hao wanatakiwa kuwapa haki zao kama wafanyakazi wengine wa maofisini.

Bibi Fatuma Mbwana”Mimi ni jirani yake Celina naona jinsi gani anavyotendewa binti huyu nimeshaongea sana na familia anyoishi nayo celina lakini kila leo naona hali ni ileile,kama mzazi nasema tujitaidi kuwajali mabinti zetu wa ndani kama watoto wetu kwasababu hali hii hikiendelea  hinasababisha kuongezeka kwa watoto mitahani na mimba katika umri mdogo”alisema.


Wafanyakazi wa ndani

Wafanyakazi wa ndani ni watu kama watu wengine na ni muhimu sana katika familia mbalimbali.

Naishi karibu na familia moja yenye watu zaidi ya saba, wakiwemo watoto  wa shule, baba na mama wenye nyumba hii pamoja na ndugu wengine wake kwa waume.

Binti wa kazi anafanya kazi kuliko zile tunazoweza kusema kama punda na nilipojaribu kudodosa mshahara wake ananiambia analipwa shilingi 15,000 kwa mwenzi.

Mfanyakazi  huyu anakuwa wa kwanza kuamka na wamwisho kulala kila siku,hakai sebuleni hali pamoja na wanafamilia hiyo,haendi likizo na anapovunja chombo hukatwa kwenye mshahara wake.

Tabia na mwenendo wa mwajiri wake ambaye ni mtu mwenye uwezo tu ulinishangaza na kunisikitisha nikajiuliza,haya ndiyo maisha anayopaswa kupewa mfanyakazi huyu?

Huu ni ubaguzi  na matokeo yake wanatoroka na kwenda kusikojulikana na hivyo tunakuwa tumewaharibia kabisa maisha.Kazi za ndani ni kazi kama zilivyo kazi nyingine ukosefu wa elimu walionao hawa isiwe kigezo cha kuwabagua na kuwanyima haki zao,kuwanyanyasa na kuwafanya kama watumwa wa enzi za ukoloni.