WATOTO WA JINSIA YA KIKE

Watoto wa jinsia ya kike ni watoto kama wengine na wana haki sawa na watoto wengine katika jamii.Lakini kuna baadhi ya wanajamii wanabagua watoto wa jinsia ya kike na kupendelea jinsia ya watoto wa kiume.

Tukiangalia baadhi ya jamii na baadhi ya familia bado wanatumia tamaduni za kizamani wanawapa kipaumbele sana watoto wa kiume na sio watoto wa kike.Wakisema watoto wa kike wapo kwa ajili ya kuolewa na kufanya kazi za nyumbani.

Nakuamini watoto wakike hawatakiwi kupata elimu watoto wakiume ndio wanaopaswa kusoma kwasababu ukimsomesha mtoto wa kike utapata hasara lakini ukisomesha mtoto wa kiume ndio unasomesha familia nzima.

Haki za watoto za jinsia zote wanazotakiwa kupata ni maradhi,elimu,chakula na muda wa kupumzika,ivyo vyote watoto wote wanatakiwa kuvipata.Pia ata kazi za nyumbani wanatakiwa kusaidiana kwasababu hamna sehemu ambayo imeandikwa kazi hizi za mtoto wa kike na hizi za mtoto wa kiume.

Kinachotakiwa jamii na ata familia zinatakiwa kuwa na upendo kwa watoto wote na sio kubagua huyu wa kike huyu wa kiume watoto wote sawa.Pia inasaidia kujenga familia bora na ata kujenga taifa la kesho kwa sababu watoto wote ndio nguvu kazi ya baadae.


watoto

Watoto kwa ujumla ni mchango na pia ni tegemezi katika jamii yetu ya leo.Nitegemezi kwasababu mtoto ni nguvu kazi ya baadae katika kuinua na kuleta maendeleo.Lakini kuna ubaguzi unaofanywa na wanajamii kwa watoto ambavyo havimpi huru.

Mambo ambayo mtoto/watoto wanabaguliwa katika jamii ni yafuatayo

  1. HAKI YA WATOTO- watoto wengi hawapati haki zao katika jamii yetu tukiangalia katika familia watoto hawapewi nafasi ya kujielezea kuhusina na vitu vya familia,mfano utakuta familia yake inamgogoro na anaona tatizo ni nini lakini akijaribu kuliongelea ataambiwa havimuhusu wakati na yeye ni wa familia.Ata katika vikao vya familia mtoto/watoto huwa hawa pewi nafasi ya kuchangia chochote kinachousiana na kikao icho.
  2. ELIMU-tatizo ili linasababisha watoto kukimbilia mtaani kwasababu kuna baadhi ya familia wanabagua kutoa elimu kwa baadhi ya watoto.Pia katika jamii yetu/nchi yetu elimu inayotolewa ni ya kulazimishana kwasababu utakuta mtoto anapenda mpira,muziki lakini apati nafasi ya kuvisomea ivyo vitu na kudai vitampotezea muda.

    Elimu ni haki kwa watoto wote.